Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Zuchu, ametangaza kuwa uhusiano wake wa ndoa na Diamond Platnumz umefikia tamati.
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mitandao ya kijamii, Zuchu amesema wameamua kuhitimisha ndoa yao kwa makubaliano ya pande zote.Ameeleza kuwa licha ya kuachana kama wanandoa, wataendelea kushirikiana katika masuala ya kazi na muziki.












