Magazeti leo Septemba 1,2026

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA), Profesa Raphael Chibunda, amesema panya Magawa, aliyefunzwa na SUA kwa kushirikiana na shirika la APOPO, ameacha historia kubwa nchini Cambodia baada ya kusaidia kugundua mabomu ya ardhini na hatimaye kujengewa mnara wa kumuenzi katika mji wa Siem Reap.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma Agosti 31,2026, Profesa Chibunda amesema panya wanaotumika katika mradi huo ni panya wa asili wa Tanzania, ambao awali walikamatwa katika milima ya Uluguru mkoani Morogoro na sasa wanaendelea kuzalishwa na kufundishwa katika kituo hicho.

Amesema SUA imeweka mfumo maalumu wa kuwahudumia panya hao katika hatua mbalimbali za maisha yao, kuanzia kuzaliwa, mafunzo hadi kustaafu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here