Magazeti leo Septemba 4,2026

Bunge limeridhia azimio la kuridhia Mkataba wa Uanzishwaji wa Taasisi ya Ukuzaji wa Maendeleo ya Kijani Duniani (GGGI) lililowasilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni bungeni jijini Dodoma, Septemba 03, 2026.
Kupitia Mkataba huo Tanzania itapata manufaa yakiwemo kuongeza uwezo wake katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kukuza uchumi unaolenga kuzingatia hifadhi ya mazingira.

Awali akiwasilisha maelezo hayo, alisema Taasisi ya kimataifa ya ikilenga kushirikiana na nchi wanachama katika uandaaji wa miradi ya uhifadhi wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi; kusaidia taasisi za ndani za nchi wanachama kupata ithibati katika usimamizi wa fedha za Mifuko.

GGGCI upatikanaji wa fedha za misaada na mikopo yenye riba nafuu kwa nchi pamoja na uwekezaji kwenye hati fungani za kijani utaongezeka na hivyo kuchochea mazingira endelevu kwa ustawi wa nchi.


















Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here