Magazeti leo Septemba 3,2026

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Kamishna Msaidizi wa Polisi Salim Morcase jana Septemba 2, 2026 amewataka maafisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wilayani Bagamoyo kufanya kazi kwa weledi na uadilifu.
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na askari katika kikao kazi ambapo amewataka askari kuzingatia mwenendo mwema wa utendaji kazi wenye kuzingatia nidhamu, haki, weledi na uadilifu ili kutoa huduma bora kwa wateja na jamii wanayoihudumia.

Akizungumza katika kikao hiko, Kamanda Morcase amewataka askari kuwa na tabia njema na nidhamu wanapokuwa wanawahudumia wateja pasipo kujali hali zao na masharti yaliyo nje ya utaratibu wa Haki Jinai ili kuepusha malalamiko yanayoepukika na kuleta tija katika kutekeleza majukumu yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here