Makamu wa Rais Dkt.Nchimbi afanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya OACPS

ARUSHA-Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) Mhe. Moussa Saleh Batraki, mazungumzo yaliyofanyika jijini Arusha.
Katika Mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amemuhakikishia Katibu Mkuu wa OACPS dhamira ya Tanzania kuendelea kutoa ushirikiano kwa Taasisi hiyo katika kuleta mageuzi na kuifanya kuwa na tija kwa nchi wanachama.

Aidha amempongeza Katibu Mkuu wa Jumuiya ya OACPS kwa kutekeleza ajenda ya mageuzi ikiwa ni pamoja na kuongeza uadilifu na kupunguza utegemezi kwa lengo la kufanya Taasisi hiyo kuwa na nguvu zaidi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Afrika, Karibiani na Pasifiki (OACPS) Mhe. Moussa Saleh Batraki ameeleza kuhusu vipaumbele vya Taasisi hiyo ikiwemo suala la kuimarisha biashara, kuimarisha mtangamano miongoni mwa nchi wanachama, kujenga uhimilivu katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Pia ameeleza dhamira ya Taasisi hiyo ya kuweka kipaumbele na uwekezaji katika TEHAMA, hususani katika teknolojia za kidijitali, akili unde, ulinzi na usimamizi wa takwimu na taarifa.

Pia kuimarisha mahusiano ya kibiashara miongoni mwa nchi zinazoendelea pamoja na kuwajengea uwezo wanawake katika masuala ya kiuchumi.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji na Umoja wa Ulaya Mhe. Jestas Nyamanga pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Ellen Maduhu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here