Magazeti leo Septemba 11,2026

Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeendelea kusogeza huduma na elimu kuhusu viwango, ubora na usalama wa bidhaa karibu na wananchi kupitia Kliniki ya Viwango, hatua inayolenga kurahisisha upatikanaji wa huduma hizo na kuwawezesha wafanyabiashara kuzingatia matakwa ya viwango.
Akizungumza wakati wa Kliniki hiyo inayoendelea Kariakoo na Mwenge Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Salum Yusuph, kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Kinondoni ameipongeza TBS kwa kuendelea kuwafikishia wananchi huduma hizo, akisema zina mchango mkubwa katika kuhakikisha bidhaa zinazozalishwa, kusambazwa na kuuzwa nchini zinakidhi viwango vinavyotakiwa.

Yusuph amesema huduma zinazotolewa na TBS, ikiwemo upimaji, ukaguzi, usajili wa bidhaa na majengo pamoja na elimu kwa umma, ni muhimu katika kulinda afya za wananchi na kujenga imani katika bidhaa zinazouzwa sokoni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here