Mshikamano katika kudumisha amani,ulinzi na usalama wa wananchi

RUKWA-Vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Rukwa vimefanya mazoezi ya pamoja ya matembezi na kukimbia mbio za pole (jogging) ikiwa ni sehemu ya kuimarisha mshikamano baina ya taasisi hizo na kuongeza ushirikiano katika kudumisha amani, ulinzi na usalama wa wananchi.
Mazoezi hayo yamefanyika Julai 17, 2026, yakianzia katika Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa na kupita katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Sumbawanga. Yameongozwa na Katibu Tawala wa Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga Gabriel Masinga aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga.
Mbali na vyombo vya ulinzi na usalama, wananchi mbalimbali walishiriki mazoezi hayo, jambo lililoonesha mshikamano na kuimarisha uhusiano kati ya wananchi na vyombo vyao vya ulinzi na usalama. Ushiriki huo umeendelea kujenga imani, ushirikiano na dhana ya usalama shirikishi katika jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here