Spika wa Bunge Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb) amesema Bunge la Tanzania limechukua hatua madhubuti za kuhimiza matumizi ya magari ya umeme pamoja na gesi.
Amesema hatua hizo zimelenga kuimarisha utekelezaji wa mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ili kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).
Mheshimiwa Spika ameyasema hayo Julai 14, 2026 wakati akiwasilisha taarifa ya Bunge la Tanzania kuhusu matumizi ya Nishati Safi kwenye Jukwaa la Kibunge katika Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Malengo ya Maendeleo Endelevu (HLPF) 2026.
Mkutano huo umefanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa (UN), jijini New York, nchini Marekani.
Amesema Bunge la Tanzania limepitisha marekebisho ya sera na sheria za kodi yaliyopunguza ushuru wa magari ya umeme kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 na kwamba misamaha mbalimbali ya ushuru na kodi kwa baadhi ya magari yanayotumia umeme na gesi imetolewa ili kuongeza matumizi ya usafiri rafiki kwa mazingira.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo






























