Mwanasheria Mkuu wa Serikali ashiriki ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa Mwaka wa Taasisi ya Wasuluhishi Tanzania (TIArb) na Wiki ya Usuluhishi ya Dar es Salaam,atoa neno

DAR-Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Hamza S.Johari amesema, Tanzania inalenga kujijenga kuwa kituo muhimu cha usuluhishi wa migogoro ya uwekezaji na biashara ndani na nje ya nchi, hatua inayolenga kuimarisha mazingira ya biashara,kuvutia uwekezaji na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Mheshimiwa Johari ameyasema hayo leo Julai 22,2026 jijini Dar es Salaam wakati akitoa salamu kwa washiriki wa hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa Nane wa Mwaka wa Taasisi ya Wasuluhishi Tanzania (TIArb) pamoja na Wiki ya Usuluhishi ya Dar es Salaam (Dar Arbitration Week).

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Dkt. Mustapher Mohamed Siyani, akimuwakilisha Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania.

Amesema, ofisi yake inatambua umuhimu wa usuluhishi katika kutatua migogoro inayohusu uwekezaji na biashara,akieleza kuwa mfumo huo ni muhimu katika kujenga mazingira salama,ya kuaminika na yenye kutabirika kwa wawekezaji na wafanyabiashara.
Pia,amesema uwepo wa mifumo madhubuti ya kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi ni miongoni mwa mambo yanayoweza kuongeza imani ya wawekezaji katika kufanya shughuli zao nchini, kwa kuwa unawapa fursa ya kupata suluhisho la migogoro kwa njia yenye ufanisi, utaalamu na kwa wakati.

Kwa mujibu wa Mheshimiwa Johari, usuluhishi una nafasi kubwa katika kuchochea maendeleo ya sekta ya biashara na uwekezaji, kwa kuwa migogoro inaposhughulikiwa kwa ufanisi, huwezesha shughuli za kiuchumi kuendelea na kupunguza athari zinazoweza kujitokeza kutokana na migogoro ya muda mrefu.
Aidha, amesema Serikali inaendelea kupitia na kuboresha mfumo wa sheria ili kuhakikisha sheria zinakwenda sambamba na mahitaji ya sasa ya kiuchumi na maendeleo ya Taifa.

Ameeleza kuwa,katika mchakato wa kuoanisha sheria za Tanzania na malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, Sheria ya Usuluhishi ni miongoni mwa sheria zinazotarajiwa kufanyiwa maboresho.

Hatua hiyo inalenga kuhakikisha kuwa sheria zinazohusu usuluhishi hazigeuki kuwa kikwazo katika jitihada za kujenga uchumi shindani, jumuishi na unaozingatia mahitaji ya maendeleo ya Taifa.
Amesema, maboresho hayo yanapaswa kuendelea kuimarisha mazingira ya kisheria na kitaasisi yatakayowezesha migogoro ya biashara na uwekezaji kutatuliwa kwa ufanisi, huku yakilinda haki na maslahi ya pande zote zinazohusika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here