NA DIRAMAKINI
BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Sita wa mwaka 2026, yakionesha kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu, ambapo asilimia 99.92 ya watahiniwa wa shule wamefaulu.
Akizungumza wakati wa kutangaza matokeo hayo leo, Katibu Mtendaji wa NECTA, Profesa Said Ally Mohamed, amesema watahiniwa 125,056 kati ya 125,320 waliopata matokeo wamefaulu kwa madaraja ya Kwanza hadi Nne.Amesema,idadi ya watahiniwa waliopata Daraja la Kwanza imeongezeka kutoka 61,020 mwaka 2025 hadi 67,606 mwaka 2026, jambo linaloonesha kuimarika kwa ufaulu.
Kwa mujibu wa NECTA, zaidi ya asilimia 99.6 ya watahiniwa wamepata madaraja ya Kwanza, Pili na Tatu, huku karibu masomo yote yakirekodi kiwango cha ufaulu kinachozidi asilimia 93.
Aidha, Profesa Mohamed amesema,hakuna shule iliyopata wastani wa Daraja F mwaka huu, hali inayodhihirisha kuendelea kuimarika kwa matokeo ya elimu ya sekondari nchini.
Haya hapa Matokeo ya Kidato cha Sita mwaka 2026;
NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA
ACSEE 2026 EXAMINATION RESULTS ENQUIRIES
CLICK ANY LETTER BELOW TO FILTER CENTRES BY ALPHABET |