Rais Dkt.Samia amjulia hali mlezi wa Mwenyezi wa ACT Wazalendo,ampa pole Pacome katika Hospitali ya Aga Khan

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan amemjulia hali Sheikh Rashid Hamad Othman mlezi wa Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo, Mhe.Othman Masoud Othman, ambaye anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.
Akiwa hospitalini hapo, Rais Dkt.Samia pia amearifiwa kuhusu uwepo wa mchezaji wa Klabu ya Young Africans (Yanga), Pacome Zouzouaq aliyekuwa amelazwa katika chumba jirani.

Rais alipata fursa ya kumtembelea Pacome na kumpa pole kufuatia majeraha aliyoyapata katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Young Africans na JKT Tanzania uliochezwa hivi karibuni kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, jijini Dar es Salaam.
Hatua hiyo imeonesha moyo wa Rais Samia wa kuwajulia hali wagonjwa na kuwafariji katika kipindi wanachopitia changamoto za kiafya.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here