Umoja wa Mataifa wawatunuku Nishani maafisa wawili wa Jeshi la Polisi nchini Tanzania

ABYEI-Jeshi la Polisi Tanzania limeendelea kufanya vyema katika Operesheni za kulinda amani duniani baada ya maafisa wake wawili kutunukiwa nishani na cheti cha pongezi na Umoja wa Mataifa kwa mchango wao katika kulinda amani katika eneo la Utawala Maalum la Abyei, lililopo mpakani mwa Sudan na Sudan Kusini.
Maafisa hao ni Mrakibu wa Polisi (SP) Shida Lugoye na Mkaguzi wa Polisi Ajara Kashozi ambao wote wametumikia katika dhamana ya Police Advisor tangu Julai 2024.

Nishani na vyeti hivyo vimetolewa na Umoja wa Mataifa tarehe 21 Julai 2026 ikiwa ni ishara ya kuthamini utendaji kazi bora, uadilifu na uzalendo walioonesha katika kipindi chote cha utumishi wao katika eneo lenye mgogoro.
Akizungumzia mafanikio hayo, Kamishna wa Polisi Ms. Helmey H.L Abraham, ambaye amewakabidhi nishani hizo kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amepongeza juhudi za maafisa hao katika kudumisha amani, kulinda raia na kushirikiana na jamii ya kimataifa ili kuleta utulivu katika Eneo la Abyei.

Pamoja na Tanzania, nchi nyingine zilizotunukiwa nishani na vyeti vya pongezi katika hafla hiyo ni: Urusi - 01, Misri - 01, Uturuki - 01, Gambia - 01, Tajikistan - 01 na Malawi - 01.
Jeshi la Polisi Tanzania limeendelea kuchangia kwa kiasi kikubwa katika harakati za kulinda amani duniani chini ya bendera ya Umoja wa Mataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here