Wananchi wa Tengeru waishukuru Serikali kwa ujenzi wa barabara

ARUSHA-Wananchi na wafanyabiashara wa eneo la Tengeru katika Halmashauri ya Meru wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ujenzi wa barabara hiyo ya Tengeru-Nambala yenye urefu wa kilomita 3.8, iliyojengwa kwa kiwango cha lami na kugharimu zaidi ya shilingi bilioni 5.
Wametoa shukrani hizo Julai 11,2026 wakati Mwenge wa Uhuru ulipotembelea na kuweka Jiwe la Msingi mradi, tukio lililoofanywa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Wazo Michael Mwang’onda.

Paulo Mbise amesema kuwa,barabara hiyo imerahisisha usafirishaji wa bidhaa zinazoletwa sokoni hapo sambamba na usafiri wa wananchi wa maeneo hayo pamoja na kurahisisha shughuli za kiuchumi na kijamii.
"Tunapongeza Serikali kwa kujenga barabara ya lami na ina mifereji ya kupitisha maji, jambo ambalo imafanya eneo hili la soko kupendeza na kuwa, kwa kweli tunashuhudia maendeleo makubwa katika maeneo mengi si hapa sokoni tuu,"amesema Josina Kitomari mfanyabiashara wa soko la Tengeru.

Juma Msechu amesema kuwa,barabara hiyo imejengwa kwa viwango bora ikiwemo mifereji ya maji ya mvua inayosaidia kudhibiti mafuriko wakati wa mvua lakini kuwa na uhakika wa barabara hiyo kupitika kwa urahisi msimu wote wa mwaka.
Awali barabara hiyo imewekwa Jiwe la Msingi na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa,Wazo Michael Mwang'onda na kusisitiza kuwa barabara hiyo inaongeza hadhi ya mji wa Tengeru.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here