Watumishi wa Wakala wa Vipimo (WMA) washiriki NBC Dodoma Marathon

DODOMA-Watumishi wa Wakala wa Vipimo (WMA) asubuhi ya leo Julai 26, 2026 wameshiriki katika mbio za NBC Marathon zilizozofanyika jijini Dodoma kwa uratibu wa Benki ya NBC.
Lengo kuu la mbio hizo ilikuwa kukusanya fedha za kusaidia matibabu kwa wagonjwa wasiojiweza, pamoja na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa mazoezi katika kuimarisha afya.

WMA imeshiriki katika mbio hizo kuunga mkono dhamira hiyo ya kibinadamu na kuonyesha mchango wa taasisi za Serikali katika masuala ya afya na ustawi wa jamii.
Katika ushiriki huo,watumishi sita wa WMA walikimbia umbali wa Kilometa 10 wakati mtumishi mmoja alikimbia Kilometa 21.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo,Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mwigulu Nchemba amewapongeza washiriki na waandaaji wa mbio hizo.
Aidha,ametoa wito kwa Watanzania kushiriki kwa wingi katika matukio kama haya ili kufanikisha malengo ya kuwasaidia wagonjwa na kuimarisha afya ya Taifa.

Akizungumza kwa niaba ya watumishi wa WMA, Meneja wa Mkoa wa Dodoma, Ibrahim Saidi amesema, "Tumeshiriki ili kusapoti lengo la NBC Marathon la kusaidia wenzetu wanaohitaji matibabu. Pia tunahamasisha Watanzania kudumisha afya kupitia mazoezi ili tuweze kutoa huduma bora kwa umma."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here