MANYARA-Agosti 7,2026 katika Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro mbele ya Mheshimiwa Charles Uisso, Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi wa Wilaya ya Simanjiro imetolewa hukumu katika shauri la jinai namba 7118/2026 dhidi ya Afisa Usafirishaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro,Bw.Ismail Khalfan Ismail.
Mshtakiwa hapo awali alikuwa anashtakiwa kwa kosa la wizi akiwa mtumishi wa umma kinyume na kifungu cha 258(1), 265 na 270 vya sheria ya kanuni ya adhabu Sura ya 16 marejeo ya mwaka 2023.
Mshtakiwa alifanya kosa hili kwa kuiba betri mbili zenye thamani ya shilingi 500,000 za magari ya Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro ambazo alizinunua kwa fedha alizokuwa amepewa na mwajiri wake ambaye ni Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro.
Mshtakiwa ametiwa hatiani na kupewa adhabu ya kutumikia kifungo cha miaka mitatu (3) gerezani au kulipa faini ya laki tano kwa mahakama pamoja na fidia ya laki tano kwa mwajiri wa mshtakiwa ambaye ni Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro.
Shauri hilo lilikuwa linaendeshwa na mwendesha mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),Wakili Faustin Mushi.
Tags
Afisa Usafirishaji
Betri za Gari
Habari
Mahakamani Leo
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
