Katibu Tawala Mkoa wa Tanga avutiwa na Sayansi ya Hali ya Hewa

MOROGORO-Katibu tawala wa Mkoa wa Tanga, Bw. Rashid Mchatta avutiwa na sayansi ya hali ya hewa, aliyasema hayo Agosti 6,2026 mara baada ya kupokea elimu ya hali ya hewa iliyokuwa inatolewa na wataalamu Bingwa wa Hali ya Hewa katika Jengo la Mamlaka lililopo katika Viwanja vya NaneNane, Morogoro kupitia maonesho ya NaneNane yanayoendelea kufanyika kuanzia tarehe 01 hadi 08 Agosti 2026.
“Sayansi ya hali ya hewa ukiifuatilia vizuri inavutia, lakini pia utaalamu wenu ni wa tofauti na sayansi nyingine, hivyo niwapongeze kwa kazi nzuri ya utabiri,"alisisitiza Bw. Mchatta.
Kupitia maonesho hayo yaliyokuwa na kauli mbiu “Tambua Soko, ongeza tija, tekeleza Dira 2050”, wageni wameendelea kupokea elimu mbalimbali ya hali ya hewa na kufahamu njia za usambazaji wa taarifa za Mamlaka, iliyopelekea wadau kuendelea kusajiliwa kupitia mifumo mbalimbali ya Mamlaka ili kuweza kupokea taarifa za hali ya hewa kidigitali.

Mamlaka inaendelea kuwaalika wadau mbalimbali kuendelea kutembelea katika mabanda ya TMA yaliyopo katika viwanja vya maonesho ya NaneNane, ambapo Kitaifa yanafanyika katika mkoa wa Dodoma na Kikanda ni katika mikoa ya Mbeya na Morogoro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here