Kwaheri X Wp Kostebo wa Polisi,Luciana Gaston Ntamakililo

NJOMBE-Picha mbalimbali zikionesha shughuli za maziko ya X Wp Kostebo wa Polisi Luciana Gaston Ntamakililo yaliyofanyika Agosti 16, 2026, katika Wilaya ya Makambako mkoani Njombe ambapo Askari Polisi kutoka Mkoa ya Tarime Rorya na Njombe wameshiriki katika kuaga mwili wa marehemu X Wp Kostebo wa Polisi Luciana.
Kostebo Luciana alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza baada ya kuugua.

Wakati wa uhai wake, Kostebo Luciana alikuwa akifanya kazi katika Wilaya ya Polisi Shirati, Mkoa wa Polisi Tarime Rorya, ambako alihudumu kwa kujituma katika kulinda usalama wa wananchi.
Msiba wake umeacha huzuni kwa familia, ndugu, jamaa, askari wenzake na jamii kwa ujumla.Bwana ametoa, Bwana ametwaa; jina la Bwana lihimidiwe.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here