SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limeweka Viwango vya Chini vya Ufanisi wa Nishati (MEPS) kwa vifaa vinavyotumia umeme, hatua inayolenga kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya nishati na kuwasaidia wananchi kupata vifaa bora na vyenye ufanisi mkubwa.
Aliyasema hayo Agosti 18, 2026 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Candida Shirima, wakati akifungua mafunzo kuhusu viwango vya ufanisi wa nishati na uwekaji wa alama za ufanisi kwa vifaa vya kupikia vya majumbani vinavyotumia umeme, yaliyofanyika katika Ofisi za TBS Makao Makuu, Ubungo, Dar es Salaam.Alisema viwango hivyo vimeweka kiwango cha chini cha ufanisi ambacho vifaa vya umeme vinapaswa kufikia ili kupunguza matumizi makubwa yasiyo na tija ya umeme.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo











