DODOMA-Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Mheshimiwa Hamza S. Johari amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Taasisi ya Women Insipire Women ofisini kwake bungeni jijini Dodoma tarehe 18 Agosti, 2026.
Taasisi ya Women Inspire Women inajishughulisha na kuwawezesha wanawake, wasichana, watoto na makundi maalumu kupitia Elimu ya Sheria, uhamasishaji na huduma za kijamii.
Uongozi wa taasisi hiyo umemtembelea Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa lengo la kujitambulisha na kueleza majukumu ya taasisi hiyo.
Ziara ya hiyo imeongozwa na Mwenyekiti wa taasisi hiyo,Bi.Letitia Ntagazwa aliyeambatana na Katibu,Bi. Rosemary Mwaipopo na Mhasibu Msaidizi,Bi.Suzan Mwaitenda.
