Michezo yaimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na China,Msigwa afungua mashindano ya kikapu

DAR-Sekta ya michezo imekua daraja la kuimarisha urafiki, mshikamano na ushirikiano kati ya Tanzania na China kupitia ushirikiano kwenye sekta hiyo ikiwemo uwekezaji katika miundombinu, biashara na elimu.
Hayo yamesemwa Agosti Mosi,2026 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati akifungua Mashindano ya 13 ya Mpira wa Kikapu ya Chama cha Wafanyabiashara wa China (Tanzania) katika viwanja vya Don Bosco vilivyopo Oysterbay, Dar es Salaam.

Msigwa amesema, Tanzania na China zina ushirikiano wa muda mrefu, ambao umeleta maendeleo kwa nchi hizo, huku akiishukuru Serikali ya China kwa mchango wake katika sekta ya michezo nchini na kuhimiza uwekezaji zaidi kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Kwa upande wake Balozi wa China hapa Bi. Chen Mingjian, alisema michezo inaendelea kuimarisha uhusiano wa kihistoria kati ya Tanzania na China, huku Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa China nchini Tanzania, Jiang Yuntao, akiishukuru Serikali ya Tanzania na Ubalozi wa China kwa kuendelea kuwezesha kufanyika kwa mashindano hayo kila mwaka.
Mashindano hayo yameanza Agosti 1 hadi 8, 2026 na yanasimamiwa na Chama cha Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) kwa kuzingatia kanuni za FIBA ambapo yanakutanisha Kampuni mbalimbali za Kichina zinazofanya shughuli zake hapa nchini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here