MwanaHALISI lakiri kupokea barua ya kusitisha leseni yake kwa miezi sita

GAZETI la MwanaHALISI limekiri kupokea barua kutoka Idara ya Habari-MAELEZO inayomtaarifu Mhariri Mtendaji, kuhusu uamuzi wa kusitisha leseni yake kwa kipindi cha miezi sita, kuanzia tarehe 19 Agosti 2026.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Agosti 21,2026 na Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo,Bw.Saed Kubenea.

Katika barua hiyo, Idara ya Habari MAELEZO imeainisha hoja mbalimbali kuhusu baadhi ya habari zilizo chapishwa na MwanaHALISI na kuhitimisha kuwa gazeti limekiuka misingi ya uandishi wa habari.

"MwanaHALISI halikubaliani na hitimisho hilo. Tangu kuanzishwa kwake Aprili 2006, gazeti limejikita katika uandishi wa habari unaogusa masuala yenye maslahi kwa umma, hususan habari za uchunguzi, uwajibikaji wa taasisi za umma na matumizi ya rasilimali za nchi.

"MwanaHALISI linatambua na kuheshimu sheria za nchi na wajibu wa kila chombo cha habari kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na misingi ya taaluma."

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo wanaamini katika uhuru wa habari, haki ya wananchi kupata taarifa na wajibu wa vyombo vya habari kuhoji, kuchunguza na kukosoa masuala yenye maslahi kwa umma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here