Mwanasheria Mkuu wa Serikali awasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria kwa Kamati ya Bunge leo

DODOMA-Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Hamza S.Johari leo Agosti 11,2026 bungeni jijini Dodoma amewasilisha Maelezo ya Serikali kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na.2) wa Mwaka 2026 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments ) (No.2) Bill, 2026 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala,Katiba na Sheria.
Aidha, Mheshimiwa Johari ametoa maelezo ya Serikali kuhusiana na Muswada huo unaolenga kufanya marekebisho katika Sheria kama vile Sheria ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Sura ya 166, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Wilaya) Sura ya 287, Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji), Sura ya 288, Sheria ya Baraza la Usalama la Taifa, Sura ya 61, Sheria ya Uthamini na Usajili wa Wathamini, Sura ya 138 na Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori, Sura ya 283.
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria inayoongozwa na Mwenyekiti Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) imepokea na kujadili maelezo Serikali kuhusiana na Muswada huo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here