PEMBA-Waumini wa dini ya Kiislamu wametakiwa kuendelea kuitunza amani ya nchi kwa kuepuka makundi yanayohamasisha uvunjivu wa amani ili taifa liweze kupiga hatua za kimaendeleo sambamba na kulinda utu wa mwanamke na watoto.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Polisi jamii Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Makame Ali Makame, wakati alipokuwa akizungumza na waumini wa dini ya kiislamu waliofika katika msikiti wa Kilindini, shehia ya Mapofu kwa ajili ya ibada.
ASP Makame ameongeza kuwa, bila ya amani hakuna maendeleo hivyo amewataka waumini hao kuendelea kukumbushana umuhimu wa kutunza amani miongoni mwao ili wanawake na watoto wabaki salama kwani pasipo na amani kundi hilo ndio linaloteseka.
