NA DIRAMAKINI
MABINGWA wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Yanga SC ya jijini Dar es Salaam wametwaa Ngao ya Jamii baada ya kuwachapa watani zao wa jadi, Simba SC ya jijini Dar es Salaam bao 1-0.
Ni kupitia mtanange wa aina yake ambao ulikuwa na mvuto mkubwa uliopigwa leo Agosti 12, 2026 katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa na mshambuliaji, Albert Kangwanda akimalizia krosi iliyochongwa na beki wa kushoto, Chedrack Boka.


Mchezo huu umekuwa kipimo cha kwanza cha nguvu za timu hizo kuelekea msimu mpya wa 2026/27, huku Yanga ikionekana kuwa na nguvu zaidi.
Katika Ngao ya Jamii ya mwaka uliopita, Yanga iliifunga Simba 1-0, bao likifungwa na Pacome Zouzoua.Aidha,Simba SC imeingia kwenye mchezo ikiwa na sura mpya na kocha mpya, Steve Barker huku Yanga nayo ikianza ukurasa mpya chini ya Manqoba Mngqithi wote kutoka nchini Afrika Kusini.