Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imepiga marufuku matangazo yote yanayohamasisha matumizi ya dawa za kupunguza au kuacha unywaji wa pombe. Dawa zilizotajwa kupigwa marufuku kutangazwa ni Naltrexone, Acamprosate na Disulfiram.
Kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa Septemba 27, 2026 na Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, Dkt. Adam Fimbo, mamlaka imebaini baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii vimekuwa vikirusha matangazo ya dawa hizo ambazo kisheria ni dawa zinazotolewa kwa cheti cha daktari pekee (Prescription-Only Medicines-POM).

Hali hiyo ni kinyume na Kanuni ya Makundi ya Dawa za Mwaka 2026 (Tangazo la Serikali Na. 150).TMDA imesema matumizi ya dawa hizo bila ushauri wa mtaalamu wa afya yanaweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo kifo, hasa zinapotumiwa pamoja na pombe au dawa nyingine.




Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

















