Makumbusho ya Taifa yalenga kufungua ukurasa mpya wa utalii wa Malikale Pangani

TANGA-Wilaya ya Pangani imeendelea kujipambanua kuwa miongoni mwa maeneo yenye historia, utamaduni na vivutio muhimu vya utalii nchini Tanzania, huku jitihada za kuviibua, kuvitangaza na kuviendeleza zikipewa msukumo mpya.
Hayo yamebainishwa leo Septemba 17, 2026, katika kikao maalumu kilicholenga kutambua, kuainisha na kuweka mikakati ya kutangaza maeneo mbalimbali ya utalii wa malikale yaliyopo Pangani.

Kikao hicho kiliongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Pangani, Bi. Ester Gama, akiwa ameambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa la Tanzania, Dkt. Noel Biseko Lwoga, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Malikale, kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Emmanuel Bwasiri na Mkuu wa Kanda ya Mashariki, Dkt. Gwakisa Kamatula.
Katika kikao hicho, viongozi hao walisisitiza umuhimu wa kuimarisha sekta ya utalii Pangani kwa kuibua na kuendeleza rasilimali zilizopo, hatua inayolenga kuifanya sekta hiyo kuwa chachu ya ukuaji wa uchumi, uundaji wa ajira na upatikanaji wa fursa kwa wananchi.

Aidha, jitihada hizo zinalenga kuitangaza Pangani kwa hadhi inayostahili, kutokana na utajiri wake wa historia, urithi wa kitamaduni na mandhari ya asili yenye uwezo wa kuvutia watalii kutoka ndani na nje ya Tanzania.
Mji wa Pangani una historia pana inayohusisha urithi wa kihistoria na kiutamaduni, sambamba na mandhari ya kuvutia yanayoweza kuifanya wilaya hiyo kuwa sehemu muhimu zaidi katika sekta ya utalii nchini.

Kwa kuibua, kuhifadhi, kutunza na kuendeleza vivutio hivyo, Pangani ina fursa kubwa ya kufungua ukurasa mpya wa maendeleo, huku wananchi wakinufaika kupitia ajira, biashara na shughuli mbalimbali zinazohusiana na utalii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here