Taasisi ya Kuthibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI) imeendelea kutekeleza shughuli za uthibiti wa ubora wa mbegu nchini kwa kutembelea Mkoa wa Manyara, Wilaya ya Babati, ambapo imefanya ukaguzi katika shamba lenye ukubwa wa ekari 25 linalozalisha mbegu za vitunguu aina ya Mang’ola Red.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TOSCI, Bw. Nyasebwa Chimagu, amesema TOSCI inaendelea kushirikiana na sekta binafsi pamoja na kuwawezesha wazalishaji wa ndani ili kuongeza uzalishaji wa mbegu nchini na kupunguza utegemezi wa mbegu zinazoagizwa kutoka nje ya nchi.
Amesema Serikali inaendelea kuweka msisitizo katika uzalishaji wa mazao ya bustani, hususan mboga mboga na viungo kama vitunguu, ambayo ni miongoni mwa mazao yanayotoa fursa za kiuchumi kwa vijana na wanawake nchini. Kwa mujibu wa Bw. Chimagu, kuongeza uzalishaji wa mbegu bora ndani ya nchi kutasaidia kuimarisha upatikanaji wa mbegu kwa wakulima na kuongeza tija katika kilimo.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo






























