DOHA-Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Jumatatu, Septemba 28, 2026, amefanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Qatar ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar, Sheikh Mohammed bin Abdulrahman bin Jassim Al Thani, katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Qatar jijini Doha.
Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamejadili masuala mbalimbali yanayolenga kuimarisha na kukuza uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Qatar.
Dkt.Mwigulu na ujumbe wake wamepokelewa katika Ofisi ya Waziri Mkuu wa Qatar ikiwa ni sehemu ya ratiba ya ziara yake ya kikazi nchini Qatar.Ziara hiyo inaendelea kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na ushirikiano wa Tanzania na Qatar, pamoja na kufungua fursa zaidi za ushirikiano katika maeneo mbalimbali ya maendeleo na uwekezaji.
