MWANASHERIA Mkuu wa Serikali,Mheshimiwa Hamza S. Johari leo Septemba 7,2026 amesaini Kitabu cha Maombolezo katika msiba wa Mheshimiwa Hafidh Ameir Hassan ambaye alikuwa mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Mheshimiwa Hafidh Ameir Hassan amefariki dunia leo Septemba 7, 2026 akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Kumbukumbu ya Emilio Mzena, Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Makamu wa Rais wa Tanzania,Mheshimiwa Deogratius Ndejembi, Mheshimiwa Hafidh alikuwa akitibiwa ugonjwa wa moyo na alifariki dunia majira ya saa mbili asubuhi. Aidha, maziko yake yamefanyika leo huko nyumbani Kizimkazi visiwani Zanzibar.


