ADDIS ABABA-Mheshimiwa Dkt.Ngwaru Jumanne Maghembe (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ameshiriki na kuzungumza kwenye Mkutano wa Kanda ya Afrika wa Mapitio ya Nusu Muhula ya Mpango Kazi wa Doha (Doha Program of Action) uliofanyika tarehe 8 na 9 Septemba 2026 jijini Addis Ababa, Ethiopia.

Mkutano huo umewakutanisha Mawaziri na Maafisa waandamizi wa serikali za nchi za Afrika; Wawakilishi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika; na Sekta binafsi kufanya tathmini ya nusu muhula ya nchi zinazoendelea kuhusu changamoto za kimaendeleo zinazokabili nchi hizo, na namna ya kupambana na changamoto hizo kwa ajili ya kuzisaidia nchi zilizo katika kundi la nchi maskini (Least Developed Countries) kuondoka kwenye kundi hilo na kuwa nchi zenye uchumi wa Kati.
Mheshimiwa Dkt.Maghembe amehudhuria mkutano huo akimuwakilisha Mheshimiwa Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

