Viongozi wa BoT na TDB waangazia fursa za uwekezaji na maeneo ya kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo

DAR-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba amefanya mazungumzo na Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Biashara na Maendeleo (TDB), Bw. Admassu Tadesse, kuhusu fursa za uwekezaji na maeneo ya kuimarisha ushirikiano kati ya taasisi hizo.
Mkutano huo umefanyika leo, Septemba 11, 2026, kwa njia mseto, ambapo Gavana Tutuba na Naibu Gavana, Dkt. Rahma Mahfoudh, walishiriki kwa njia ya mtandao, huku Naibu Gavana, Dkt. Yamungu Kayandabila, baadhi ya viongozi wa Benki Kuu pamoja na ujumbe wa TDB wakishiriki ana kwa ana katika Ofisi ya Benki Kuu jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, pande hizo mbili zilijadili fursa za kuimarisha ushirikiano kati ya TDB, BoT na taasisi nyingine za fedha nchini, hususan katika kuwezesha uwekezaji, kuongeza upatikanaji wa fedha na kuchochea maendeleo ya uchumi nchini.

Gavana Tutuba aliishukuru TDB kwa ushiriki wake na kwa kuwasilisha maeneo ya fursa na masuala yenye maslahi ya pamoja. Alieleza kuwa mazungumzo hayo yameweka msingi muhimu wa kuendelea kutathmini fursa za ushirikiano na maeneo ambayo yanaweza kuchangia katika kuimarisha maendeleo ya sekta ya fedha na uchumi kwa ujumla.
Mkutano huo unaonesha dhamira ya Benki Kuu ya kuendelea kuimarisha ushirikiano na taasisi za fedha za kikanda kwa lengo la kukuza uwekezaji, kuimarisha upatikanaji wa huduma na mitaji, kuendeleza sekta ya fedha na kuchochea ukuaji endelevu wa uchumi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here