Waziri Mkuu kumwakilisha Rais Dkt.Samia mkutano wa Afya Moja nchini Italia

DAR-Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameondoka nchini leo Jumamosi, Septemba 19, 2026 kwenda Roma, Italia kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa siku tatu wa Kimataifa wa Kujadili Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo.
Mkutano huo utakaofanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), jijini Roma, Italia kuanzia Septemba 21–23, 2026 unalenga kuimarisha utekelezaji wa dhana ya Afya Moja (One Health) inayotambua uhusiano kati ya afya ya binadamu, wanyama, mimea na mazingira, kwa lengo la kuhakikisha mifumo endelevu ya chakula na kilimo

Mkutano huo utahusisha viongozi wa nchi na Serikali, wakiwemo Marais kati ya watano hadi saba, Mawaziri kati ya 30 hadi 50, pamoja na wawakilishi wa taasisi za kikanda na kimataifa, wadau wa maendeleo, sekta binafsi, taasisi za utafiti na mashirika ya kimataifa.
Mambo muhimu yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni Ujumuishaji wa dhana ya Afya Moja (One Health) katika sera na uwekezaji wa mifumo ya chakula na kilimo; na uimarishaji wa ushirikiano wa kisekta kati ya sekta za kilimo, mazingira, afya, fedha na mipango ya miji.

Mengine ni ukuzaji wa ubunifu, sayansi na maarifa ya ndani ili kuboresha uzuiaji wa vihatarishi, ufuatiliaji na usimamizi endelevu wa rasilimali na kuhamasisha uwekezaji na ushirikiano ili kutafsiri ahadi kuwa hatua madhubuti zenye matokeo yanayopimika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here