ZANZIBAR-Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) imezindua rasmi Mwongozo wa Mawasiliano kati ya Mzazi na Mtoto kuhusu Haki ya Afya ya Uzazi (PCC Toolkit), unaolenga kuimarisha malezi, mawasiliano, ulinzi na ustawi wa watoto na vijana.
Naibu Waziri Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto,Zawadi Amour Nassor akizindua Mwongozo wa Mawasiliano kati ya Mzazi na Mtoto kuhusu Afya ya Uzazi.Hafla ya uzinduzi imefanyika jana katika Hoteli ya Verde, Unguja , Muongozo huo umeandaliwa na UNESCO na kuikabidhi Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Zanzibar.Uzinduzi wa mwongozo huo umefanyika jana katika Hoteli ya Verde na kuzinduliwa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Zawadi Amour Nassor kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Anna Athanas Paul.
Akizungumza katika hafla hiyo, Zawadi alisema wazazi na walezi wanapaswa kuvunja ukimya katika kujadili masuala ya afya ya uzazi na watoto wao kwa kutumia lugha sahihi, yenye heshima na inayozingatia umri wa mtoto.

Alisema,watoto na vijana wanahitaji kupata taarifa sahihi zinazolingana na umri wao ili kuwasaidia kuelewa mabadiliko wanayopitia, kutambua hatari, kujilinda dhidi ya ukatili na kufanya maamuzi sahihi kuhusu maisha yao.
“Tunapozungumzia afya ya uzazi, hatuzungumzi tu masuala ya kibaolojia, bali pia malezi, maadili, mahusiano yenye heshima, usalama wa mtoto na uwezo wa kusema ‘hapana’ pale inapohitajika,”alisema.
“Tunapozungumzia afya ya uzazi, hatuzungumzi tu masuala ya kibaolojia, bali pia malezi, maadili, mahusiano yenye heshima, usalama wa mtoto na uwezo wa kusema ‘hapana’ pale inapohitajika,”alisema.Alisema,wazazi wengi wamekuwa wakihofia kuanzisha mazungumzo hayo, huku watoto wakishindwa kuuliza maswali kwa hofu ya kukemewa au kudhalilishwa, hali inayowafanya baadhi yao kutafuta taarifa zisizo sahihi kutoka kwa marafiki na mitandao ya kijamii.
“Ukimya hauondoi changamoto, bali huacha nafasi kwa upotoshaji,” alisema, akibainisha kuwa PCC Toolkit itawasaidia wazazi kuzungumza na watoto wao kwa uwazi, kusikiliza bila kutoa hukumu na kujenga mazingira ya kuaminiana.
Aidha, alisema utekelezaji wa muongozo huo unahitaji ushirikiano wa Serikali, UNESCO, mashirika ya kiraia, wazazi, walimu, viongozi wa dini na vijana wenyewe, huku akiipongeza UNESCO na wadau mbalimbali, wakiwemo Katibu Mkuu Abeda Rashid Abdallah, Mkurugenzi na Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Watoto Mohamed Jabir, kwa kuchangia maandalizi ya muongozo huo.Kwa upande wa Umoja wa Mataifa kanda ya Zanzibar akizungumza Naibu Katibu na Mratibu Dorothy Temu Usiri amesema Muongozo huo umezingatia maadili hivyo wamaimani kwamba Muungozo huyo utawazaidia wazazi kuwa na Malezi bora ya Watoto hali ambayo itawasaidia watoto kujielewa na kujifahamu mapema.
Akimwakilisha Mwakilishi Mkaazi wa UNESCO, Matias Luhanya amesema,shirika litaendelea kushirikiana na Serikali kwa ajili ya kutoa elimu na kuleta mabadiko katika Sekta ya Elimu Zanzibar kwani umepatikana muongozo wa kuwasaidia wazai.
Akizungumza mmoja kati ya wazazi, Bahati Issa kutoka Kikungwi, Unguja ameishukuru Shirika la UNESCO kwa kundaa Muongozo huo. Pia ameiomba Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kuendelea kutoa elimu dhidi ya muogozo huo kwa kila shehia ili kila mtu imfikie elimu ya Mawasiliano kati ya Mzazi na Mtoto kuhusu Haki ya Afya ya Uzazi.

