ZANZIBAR- Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amewashukuru wananchi wa Zanzibar kwa kuendelea kumwamini na kumuunga mkono katika kutekeleza majukumu yake ya kuwatumikia.
Ni wakati akitimiza mwaka mmoja tangu alipoanza kipindi cha pili cha uongozi wake katika Serikali ya Awamu ya Nane na miaka sita.
Dkt. Mwinyi amesema anaendelea kujitolea kwa moyo wote katika kuimarisha maendeleo, kuboresha maisha ya wananchi na kuhakikisha Zanzibar inajengwa kuwa eneo lenye fursa na ustawi kwa watu wote.
Amesema, dhamira yake ni kuendelea kusimamia juhudi za kuleta maendeleo yenye tija kwa wananchi, akisisitiza umuhimu wa mshikamano, ushirikiano na juhudi za pamoja katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya Zanzibar.
Rais Dkt. Mwinyi ametoa ujumbe huo katika mwaka mmoja wa kipindi chake cha pili cha uongozi, akisisitiza dhamira ya kuendelea kuwatumikia wananchi na kusukuma mbele ajenda ya maendeleo ya Zanzibar.
Tags
Baraza la Mapinduzi
Dkt. Hussein Ali Mwinyi
Habari
Habari za Zanzibar
Serikali ya Awamu ya Nane
Zanzibar










