NA DIRAMAKINI
KOCHA wa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 (Ngorongoro Heroes), Mario Campasino Rivera, ametangaza kikosi cha wachezaji 26 kitakachoingia kambini kujiandaa na michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya wenyeji Misri.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), michezo hiyo itachezwa Novemba 12 na Novemba 16, 2026 nchini Misri.
Kocha Rivera amewaita wachezaji kutoka vilabu vya ndani na vya nje ya nchi kama ifuatavyo:
Edison James kutoka Mashujaa FC, Telvin Deodatus kutoka Kagera Sugar, Roony Samwel kutoka JKT Tanzania, Ahmad Ramadhani kutoka Fountain Gate, Ismail Omar kutoka FC Polissya, Ukraine na Abdallah Hassani kutoka Azam FC.
Wengine ni Joseph Jr Michael kutoka Celta Vigo, Hispania, Godfrey Simeo kutoka Mashujaa FC, Ally Ayoub kutoka Coast Union, Rajabu Said kutoka Azam FC na Abdulnassir kutoka Yanga SC.
Pia, yumo Feisal Othman kutoka United FC, Dubai, Ridhuan Habibu kutoka Al Wasl, UAE, Issa Juma kutoka Yanga SC, Arafat Ally kutoka ENPPI SC, Misri na Mohamed Ismail kutoka AIK, Sweden.
Abdul Omari kutoka Riga FC nchini Latvia, Henry Msabila kutoka Pamba Jiji, Omary Juma kutoka Mlandege, Machupa Juma kutoka Fountain Gate, Yusuph Adam kutoka Singida BS, Suleiman Mbarouk kutoka Yanga SC na Hussein Mihambo kutoka Yanga SC.
Vilevile, kuna Hashimu Omary kutoka Fountain Gate, Faridi Yahaya kutoka Azam FC na Bakari Selemani kutoka Simba SC.
Tags
Habari
Mario Campasino Rivera
Mechi za Kirafiki
Michezo
Misri U20
Ngorongoro Heroes
Tanzania U20
TFF

