Rais Dkt. Mwinyi atembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, azindua jarida la Tanzanite

SEOUL- Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo Novemba 1, 2026 amekamilisha ziara yake nchini Korea Kusini, iliyolenga kuimarisha uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Korea katika uwekezaji, utalii, biashara na maendeleo ya kiuchumi.
Akiwa Seoul, nchini Korea Kusini Rais Dkt. Mwinyi ametembelea Ubalozi wa Tanzania na kushiriki uzinduzi wa jarida la kwanza la habari la Ubalozi, Tanzanite, linalolenga kuitangaza Tanzania na kuhamasisha fursa za uwekezaji na biashara.
Katika hafla hiyo, amempongeza Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Mhe. Noel Emmanuel Kaganda, pamoja na watendaji wa Ubalozi kwa juhudi zao za kuitangaza Tanzania na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here