NA DIRAMAKINI
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetangaza utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo, unaoonesha mawingu kiasi na mvua katika baadhi ya maeneo ya nchi, huku ikiweka angalizo la mvua kubwa kwa mikoa kadhaa kuanzia Alhamisi hadi Ijumaa wiki hii.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, tarehe 09 Novemba 2026 na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, utabiri huo unaanza saa 3.00 usiku wa leo na ni wa saa 24 zijazo kwa siku ya Jumanne, tarehe 10 Novemba 2026.
Mikoa ya Kigoma, Tabora na Katavi, pamoja na mikoa ya Kagera, Simiyu, Shinyanga, Mara, Mwanza na Geita, inatarajiwa kupata hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache, pamoja na vipindi vya jua.
Kwa upande mwingine, mikoa ya Tanga na Mtwara, visiwa vya Unguja na Pemba, pamoja na mikoa ya Manyara, Arusha na Kilimanjaro, inatarajiwa kupata hali ya mawingu kiasi na mvua nyepesi katika maeneo machache, pamoja na vipindi vya jua.
Mikoa ya Dodoma na Singida, Lindi, Dar es Salaam na Morogoro, Pwani, pamoja na mikoa ya Ruvuma, Iringa, Rukwa, Njombe, Songwe na Mbeya, inatarajiwa kupata hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Kuhusu viwango vya joto, miji ya Dar es Salaam na Dodoma inatarajiwa kuwa na joto la juu zaidi la nyuzi joto 33, huku Dodoma ikitarajiwa kushuka hadi nyuzi joto 17.
Miji mingine kama Arusha itakuwa na 28 hadi 15, Kigoma 30 hadi 20, Mbeya 27 hadi 15, Iringa 31 hadi 15, Njombe 26 hadi 12, Mwanza 30 hadi 19, Tabora 32 hadi 20, Tanga 32 hadi 23, na Zanzibar 32 hadi 23.
Upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kutoka Kusini Mashariki kwa kasi ya km 30 kwa saa kwa Pwani ya Kaskazini, na kutoka Mashariki kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani ya Kusini. Hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi madogo hadi makubwa kiasi.
Upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kutoka Kusini Mashariki kwa kasi ya km 30 kwa saa kwa Pwani ya Kaskazini, na kutoka Mashariki kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani ya Kusini. Hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi madogo hadi makubwa kiasi.TMA imesema matarajio ya siku ya Jumatano, tarehe 11 Novemba 2026, ni kuendelea kwa vipindi vya mvua katika maeneo ya Ziwa Viktoria na Magharibi mwa nchi.
Angalizo la mvua kubwa kuanzia Alhamisi
Katika matarajio ya hali mbaya ya hewa kwa siku tano zijazo, TMA imesema hakuna tahadhari kwa siku ya Jumatatu tarehe 09 Novemba 2026, Jumanne tarehe 10 Novemba 2026 na Jumatano tarehe 11 Novemba 2026.
Hata hivyo, siku ya Alhamisi tarehe 12 Novemba 2026, angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara.Siku ya Ijumaa tarehe 13 Novemba 2026, angalizo hilo litapanuka na kuhusu maeneo machache ya mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Arusha, Kilimanjaro, Manyara, Singida, Dodoma na Tabora.
Mamlaka imesema uwezekano wa kutokea kwa mvua hiyo ni wastani, na kiwango cha athari zinazoweza kutokea pia ni wastani, ambapo baadhi ya makazi yanaweza kuzungukwa na maji. Wananchi wametakiwa kuzingatia taarifa hizo na kujiandaa ipasavyo.

