Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman awasili Tanzania kwa ziara ya kikazi

DAR ES SALAAM- Waziri wa Mambo ya Nje wa Usultani wa Oman, Mhe. Sayyid Badr bin Hamad bin Hamood Albusaidi, Novemba 9, 2026 amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi.
Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mhe. Albusaidi amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo.

Katika ziara hiyo, Mhe. Albusaidi atashiriki kama Mgeni Maalumu katika Mkutano wa Tatu wa Tume ya Pamoja ya Kudumu ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Oman (Joint Permanent Commission – JPC), unaofanyika kisiwani Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here