BREAKING NEWS: Afisa wa TAKUKURU akamatwa kwa kupokea furushi la fedha


"Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Brigedia Jenerali John Mbungo, napenda kuufahamisha umma kwamba jana Septemba 10, 2020 majira ya jioni, tumemkamata Afisa Uchunguzi Mwandamizi Daraja la Pili wa TAKUKURU kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa kinyume na Kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Na.11 ya mwaka 2007;

Ameyabainisha hayo Afisa Uhusiano TAKUKURU, Doreen Kapwani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea juu ya hatua hiyo.

Amesema, Afisa Uchunguzi aliyekamatwa ni Nina Sipilon Saibul ambaye ni mtumishi katika ofisi ya TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni jijini Dar es Salaam, ambaye aliomba rushwa kwa mfanyabiashara mmoja wa jijini Dar es Salaam anayejishughulisha na shughuli za Real Estate.

"Ndugu waandishi wa habari, kama ambavyo imekuwa ikitokea kwa taarifa za watuhumiwa wengine, TAKUKURU Mkoa wa Kinondoni, ilipokea taarifa za malalamiko dhidi ya afisa wake huyo juu ya kuomba rushwa ili asiendelee na uchunguzi uliodaiwa kuwa ulikuwa ukiendelea ndani ya TAKUKURU dhidi ya mfanyabiashara huyo (mlalamikaji).

"Baada ya taarifa hizo kupokelewa, uchunguzi wa awali wa kuthibitisha tuhuma hizo ulifanyika na kubaini upo ukweli wa madai ya kuomba hongo, lakini hakukuwa na jalada wala uchunguzi wowote uliokuwa ukiendelea dhidi ya mlalamikaji.

"Baada ya TAKUKURU kujiridhisha na uchunguzi huo wa awali iliandaa mtego uliowezesha kukamatwa kwa Nina pamoja na mume wake Ramadhan Kabadi Makoye wakipokea kiasi hicho cha fedha zilizokuwa zimeombwa na Nina. TAKUKURU imechukua hatua hii ili kuhakikisha kuwa inajisafisha dhidi ya watumishi wake wachache wenye tabia ovu zenye kukichafua chombo hiki.

"Uchunguzi dhidi ya tuhuma hii unakamilishwa ili kuweza kuwafikisha watuhumiwa mahakamani mapema iwezekanavyo.Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, tunaendelea kuwashukuru wadau wengine wote ambao wamekuwa wakishirikiana nasi katika kufanikisha jukumu hili la kuzuia na kupambana na rushwa nchini kwa kutuletea taarifa za wale wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

"Tunawasihi wananchi waendelee kuiunga mkono TAKUKURU huku tukizingatia kauli mbiu yetu ya mwaka huu isemayo, "Kupambana na Rushwa ni Jukumu Langu,"amesisitiza Afisa Uhusiano TAKUKURU, Doreen Kapwani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU."Baada ya taarifa hizo kupokelewa, uchunguzi wa awali wa kuthibitisha tuhuma hizo ulifanyika na kubaini upo ukweli wa madai ya kuomba hongo, lakini hakukuwa na jalada wala uchunguzi wowote uliokuwa ukiendelea dhidi ya mlalamikaji.

"Baada ya TAKUKURU kujiridhisha na uchunguzi huo wa awali iliandaa mtego uliowezesha kukamatwa kwa Nina pamoja na mume wake Ramadhan Kabadi Makoye wakipokea kiasi hicho cha fedha zilizokuwa zimeombwa na Nina. TAKUKURU imechukua hatua hii ili kuhakikisha kuwa inajisafisha dhidi ya watumishi wake wachache wenye tabia ovu zenye kukichafua chombo hiki.Taarifa zinazofanana soma hapa.

"Uchunguzi dhidi ya tuhuma hii unakamilishwa ili kuweza kuwafikisha watuhumiwa mahakamani mapema iwezekanavyo.Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, tunaendelea kuwashukuru wadau wengine wote ambao wamekuwa wakishirikiana nasi katika kufanikisha jukumu hili la kuzuia na kupambana na rushwa nchini kwa kutuletea taarifa za wale wote wanaojihusisha na vitendo vya rushwa.

"Tunawasihi wananchi waendelee kuiunga mkono TAKUKURU huku tukizingatia kauli mbiu yetu ya mwaka huu isemayo, "Kupambana na Rushwa ni Jukumu Langu,"amesisitiza Afisa Uhusiano TAKUKURU, Doreen Kapwani kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.

No comments

Powered by Blogger.