KMC FC yaanza kujipanga dhidi ya Mwadui FC

TIMU Manispaa ya Kinondoni, KMC FC imeanza kufanya mazoezi yake ya kawaida ikiwa ni katika maandalizi ya mchezo wake dhidi ya Mwadui FC ya mkoani Shinyanga Septemba 21, mwaka huu,anaripoti CHRISTINA MWANGALA kutoka KMC FC.




KMC FC itakutana na Mwadui FC katika uwanja wa Mwadui Complex ambapo itakuwa ugenini dhidi ya mchezo huo huku ikihitaji ushindi kwa lengo la kuendelea kujiweka katika nafasi ya kuongoza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa mwaka 2020/2021.

Kupitia mazoezi hayo kikosi hicho kitaendelea kujiimarisha zaidi kwa kucheza mechi za kirafiki kabla ya kukutana na Mwadui FC jambo ambalo litaiwezesha kujiweka tayari katika mchezo huo.

Aidha, KMC hivi sasa inaongoza ligi ikiwa imejikusanyia alama sita na magoli sita katika michezo yake miwili ambapo Septemba 7,mwaka huu ilikutana na Mbeya City katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na kuibuka na ushindi wa goli nne kwa nunge, Septemba 12 ilicheza na Tanzania Prisons na kuibuka na ushindi wa goli mbili kwa moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news