Polisi wamshikilia anayedaiwa kuwakata mapanga Wana CCM Pemba

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linamshikilia Katibu wa Chama Cha ACT Wazalendo Tawi la Kosovo Shehia ya Kangani, Hassan Hamad Hassan (56) kwa tuhuma ya kuwashambulia kwa kuwakata mapanga wanachama wa Chama Cha Mapinduzi akiwemo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Wete.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mohammed Haji Hassan ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba.

 Amesema,inadaiwa kuwa mtuhimiwa huyo baada ya kutekeleza kitendo hicho alikimbia na kujificha na kwamba amelazimika kujisalimisha kituoni baada ya kutafutwa kwa siku kadhaa visiwani humo.

Pia amesema, baada ya Jeshi la Polisi kufanya upekuzi kwenye nyumba ya mtuhumiwa walikuta baadhi nyaraka zinazoonyesha kwamba huyo ni mwanachama halali wa Chama cha ACT Wazalendo.

Amesema, nyaraka hizo ni pamoja na kadi yake ya uanachama yenye namba 438052 iliyotolewa ya tarehe 20/3/2019 Wadi ya kiuyu Jimbo la Kojani visiwani humo.

No comments

Powered by Blogger.