Vijana wawili mikononi mwa polisi kwa kufungua akaunti feki za jeshi

Jeshi la Polisi nchini Uganda limewanasa vjana wawili ambao huwa wanaendesha akaunti feki za mitandao ya kijamii kwa jina la jeshi hilo huku wakilaghai wananchi, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyoonwa na Diramakini kutoka jeshi hilo imewataja vijana hao kuwa ni Mugerwa Calvin na Ochan Allan kutoka Kitebi na Nabweru.

Kupitia idara ya kushughulikia makosa ya uhalifu mitandaoni ya jeshi hilo, imethibitika kuwa vijana hao walikuwa wakiendesha akaunti za Facebook na Twitter ambapo zinalenga kudhoofisha taswira na kazi nzuri inayofanywa na jeshi kwa kusimamia ulinzi wa rai na mali zao.
Aidha kupitia taarifa hiyo, jeshi hilo limesema kuwa, lipo imara na kamwe halitaruhusu wenye nia ovu kuharibu taswira yao au kulaghai wananchi.

No comments

Powered by Blogger.