Majliwa:Nimeridhishwa na ujenzi kivuko cha Mafia

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameridhishwa na ujenzi wa kivuko cha Mafia ambacho kitatoa huduma za usafiri na usafirashaji wa abiria na mizigo kati ya Nyamisati na Mafia.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikagua maendeleo ya ujenzi wa Kivuko cha Mafia, kitakachotoa huduma kati ya Nyamisati, wilayani Kibiti na Kisiwa cha Mafia, kwenye karakana ya Songoro Marine, iliyopo Kigamboni, jijini Dar es salaam, Oktoba 5, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Ujenzi wa Kivuko hicho chenye urefu wa mita 36 na upana mita 12 umefikia asilimia 95 na kinauwezo wa kubeba abiria 200 na mizigo tani 100. Ujenzi huo umegharimu kiasi cha shilingi bilioni 5.3.

Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko hicho Oktoba 5, 2020 katika karakana ya kampuni ya Songoro Marine iliyopo Kigamboni Jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Majaliwa amesema ujenzi wa kivuko hicho ni mkakati wa Serikali katika kuendelea kujenga vivuko vinavyokwenda kwenye visiwa vilivyopo nchini.

Kivuko cha Mafia, kinachotegemea kuanza kutoa huduma mwezi ujao baada ya kukamilika kwa majaribio, kati ya Nyamisati, wilayani Kibiti na Kisiwa cha Mafia, kinachotengenezwa na Kampuni ya Songoro Marine, iliyopo Kigamboni, jijini Dar es salaam, Oktoba 5, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
“Ujumbe kwa wana-Mafia ni kwamba meli hii tunatarajia ianze kuingizwa kwenye maji kuanzia mwezi ujao, baada ya kila kazi kukamilika na TASAC kuja kujiridhisha kwamba ubora chombo hiki umekamilika, tunaamini Wana-Mafia sasa kero yao itakuwa imeisha”

Mheshimiwa Majaliwa amesema wananchi wa Mafia wanasubiri kwa hamu kuona kivuko hicho kikianza safari zake kwa ajili ya kurahisisha huduma za usafiri ikiwamo biashara.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akipokea maelezo ya ujenzi wa Kivuko cha Mafia, kitakachotoa huduma kati ya Nyamisati, wilayani Kibiti na Kisiwa cha Mafia, kutoka kwa Kaimu Meneja – TEMESA, Mkoa wa Pwani, Injinia Rehana Juma, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko hicho, kwenye karakana ya Songoro Marine, iliyopo Kigamboni, jijini Dar es salaam, Oktoba 5, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa alitoa wito kwa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) kuisaidia kampuni ya Songoro Marine kuhakikisha mzigo wa vifaa vya ukamilishaji wa kivuko hicho unapofika bandarini vinatoka haraka ili Songoro Marine wakamilishe taratibu zao.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi wa Ufundi, Kampuni ya Songoro Marine, Khalid Songoro, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Kivuko cha Mafia, kitakachotoa huduma kati ya Nyamisati, wilayani Kibiti na Kisiwa cha Mafia, kwenye karakana ya Songoro Marine, iliyopo Kigamboni, jijini Dar es salaam, Oktoba 5, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mheshimiwa Majaliwa aliongeza kuwa ujenzi wa vivuko hivyo unawapa uhakika Watanzania wa kuunganishwa na maeneo yote nchini ili kuendelea kufanya shughuli zao za kiuchumi, kurahisisha mawasiliano na kurahisisha gharama za usafiri.

Vilevile, Mheshimiwa Majaliwa aliipongeza kampuni ya Songoro Marine kwa ujenzi wa vivuko vyenye ubora wa hali ya juu na kwamba kwa sasa Serikali inauhakika na kampuni ya utengenezaji wa vivuko nchini kwa sababu ya uwezo wake wa kukamilisha kazi kwa wakati na ubora.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi wa Ufundi, Kampuni ya Songoro Marine, Khalid Songoro, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Kivuko cha Mafia, kitakachotoa huduma kati ya Nyamisati, wilayani Kibiti na Kisiwa cha Mafia, kwenye karakana ya Songoro Marine, iliyopo Kigamboni, jijini Dar es salaam, Oktoba 5, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi wa Ufundi, Kampuni ya Songoro Marine, Khalid Songoro, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Kivuko cha Mafia, kitakachotoa huduma kati ya Nyamisati, wilayani Kibiti na Kisiwa cha Mafia, kwenye karakana ya Songoro Marine, iliyopo Kigamboni, jijini Dar es salaam, Oktoba 5, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akifafanuliwa jambo na Mkurugenzi wa Ufundi, Kampuni ya Songoro Marine, Khalid Songoro, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Kivuko cha Mafia, kitakachotoa huduma kati ya Nyamisati, wilayani Kibiti na Kisiwa cha Mafia, kwenye karakana ya Songoro Marine, iliyopo Kigamboni, jijini Dar es salaam, Oktoba 5, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akikagua maendeleo ya ujenzi wa Kivuko cha Mafia, kitakachotoa huduma kati ya Nyamisati, wilayani Kibiti na Kisiwa cha Mafia, kwenye karakana ya Songoro Marine, iliyopo Kigamboni, jijini Dar es salaam, Oktoba 5, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news