Rais Dkt.Mwinyi asema ana imani kubwa na uongozi wa Rais Magufuli

Rais wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali hassan Mwinyi ameupongeza utayari wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli wa kuahidi kuwa mstari wa mbele kumsaidia katika kutekeleza yale yote aliyoyaahidi wakati wa kampeni,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Rais Dkt. Hussein Mwinyi ameyasema hayo leo Novemba 16, 2020 wakati akitoa salamu zake katika hafla ya kuapishwa kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa pamoja na mawaziri akiwemo Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, na Waziri wa Mmabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profsa Kabudi hafla iliyofanyika katika Ikulu ya Chamwino, nje kidogo ya Jiji la Dodoma.

Mapema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli aliwaapisha viongozi hao na baadae baadhi ya viongozi walipata nafasi ya kutoa salamu zao akiwemo Rais Dkt. Hussein Mwinyi.

Akitoa salamu zake hizo, Rais Dkt. Hussein Mwinyi ameeleza imani kubwa aliyonayo Rais Magufuli kwake hatua ambayo inaonesha matarajio ya wananchi kwa kiongozi wao huyo pamoja na Serikali yao ya Mapinduzi ya Zanzibar. Amesema kuwa, wananchi wa Zanzibar walikuwa na mategemeo makubwa kwa maisha yao bora baada ya uchaguzi mkuu.


Hivyo, matumaini hayo yamezidi kuimarika na kupanda mara baada ya kusikia hotuba ya Rais Magufuli katika ufunguzi wa Bunge la 12 wakati alipoahidi kuwa katika miaka mitano ijayo Seriali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itatoa ushirikiano mkubwa na kufanya kazi kwa karibu na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Aidha, amesema kuwa wananchi hao wamezidi kupata matumaini kutokana na azma ya Rais Magufuli ya kuendelea kuisaidia na kuiunga mkono Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hivyo, Rais Dkt. Hussein Mwinyi aliahidi kufanya kazi na kushirikiana na Rais Magufuli kwa azma ya kuleta maendeleo kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Amempongeza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa pamoja na Mawaziri wawili walioapishwa akiwemo Waziri wa Fedha na Mipango Philip Hisdori Mpango pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Afrika Mashariki Profesa Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi.

Rais Hussein Mwinyi amempongeza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majali Majaliwa kwa utendaji wake mzuri wa kazi hivyo kupata nafasi hiyo ni stahiki yake kwani aliwahi kwua bosi wake hivyo anautambua vyema utendaji wake.

Aidha, amempongeza Waziri Palamagamba John Aidan Mwaluko Kabudi na kueleza kwamba kwa vile suala la Mambo ya Nje ni la Muuungano hivyo, anaimanikuwa kuwa atafanya kazi nae kwa mashrikiano makubwa.


Rais Dkt. Hussein Mwinyi amesema kuwa anaimani kubwa ya uongozi wa Waziri Philip Hisdori Mpango katika masuala ya fedha hasa ikizingatiwa kwa Zanzibar na Tanzania Bara zinategemeana hivyo alimuahidi kushirikiana nae.

Rais Magufuli amempongeza Waziri Mkuu pamoja na Mawaziri wote walioapa huku akieleza kwamba hakuwa na haraka ya kuwachagua Mawaziri kwani bado mda upo hasa aikizingatiwa kwamba mara hii wako wengi. Amewataka wabunge wasiwe na presha kwani kaziwaliyoomba ni Ubunge na sio Uawaziri hivyo waendelee kufanya kazi yao hiyo.


Hata hivyo, amewataka viongozi hao kwenda kuwatumikia wananchi kwani wananchi wameonesha imani kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi Tanzania Bara na Zanzibar hiyo imeoesha wazi kutokana na asilimia kubwa ya ushindi uliopatikana kwa Urais wa Zanzibar, Urais wa Jamhuri ya Muunganao wa Tanzania pamoja na viongozi wote waliogombea kwa tiketi ya CCM.

Nae Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameeleza imani aliyonayo Rais Magufuli kwa viongozi hao wote aliowateua inatokana na jinsi walivyomsaidia katika uongozi wake wa kipindi cha miaka mitano ilyopita.

Ameongeza kuwa katika uongozi wa Rais Magufuli hasa katika kipindi cha miaka miwili ya mwanzo aliwanyoosha vizuri na kukubali kwamba walinyooka na kukiri kuwa hivi sasa wamekuwa walimu wazuri na hivi sasa wanauwezo mkubwa wa kuwaongoza wenzao.

Mapema Rais Magufuli amemuapisha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa pamoja na Mawaziri wenzake hao wawili ambao walikula kiapo, walisaini kiapo pamoja na kula kiapo cha uadilifu kwa uongozi wa umma huku kila mmoja akitoa salamu zake Hafla hiyo imetumbuizwa na Brasbandi ya Polisi pamoja na burudani za msainii maarufu Masanja Mkandamizaji.

Post a Comment

0 Comments