Tetesi:Everton na Tottenham zinamtaka Arkadiusz Milik

Klabu ya Everton na Tottenham kwa pamoja zinataka kumsaini mshambuliaji wa timu ya Napoli, Arkadiusz Milik (26).
Kwa mujibu wa Sun, Milik anaweza kupatikana kwa pauni milioni 10 tu katika kipindi cha dirisha la uhamisho wa wachezaji mwezi Januari,mwakani.

Wakati huo huo, 90 min inaripoti kuwa, Celtic wanataka kumsaini mlinda lango wa Manchester United na England Dean Henderson (23) kwa mkataba wa mkopo mwezi Januari huku Barcelona wanaangalia uwezekano wa kumchukua beki wa Arsenal na Ujerumani, Shkodran Mustafi.

Aidha, 90min inaripoti kuwa, Manchester United bado wanamtaka winga wa Borussia Dortmund na England, Jadon Sancho (20) na wanajaribu pia kusaini mkataba wa kumleta kabla ya mshindano ya michuano ya mwaka ujao ya kombe la Ulaya -European Championships.

Kwa mujibu wa Goal, Klabu ya Paris St-Germain wanaandaa dau kwa ajili ya mlinzi wa Real Madrid na Uhispania, Sergio Ramos (34) huku PSG wanajaribu kuongeza mikataba ya Mfaransa, Kylian Mbappe (21) na mshambuliaji Mbrazil, Neymar da Silva Santos JĂșnior au Neymar (28).

Post a Comment

0 Comments