Tshala Muana akamatwa kwa wimbo unaodaiwa kumkejeli Rais

Shirika la Kutetea Haki za Binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo la ACAJ limewataka maafisa wa usalama nchini humo kumwachilia huru mwanamziki maarufu Tshala Muana ambaye alikamatwa jana mjini Kinshasa, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Polisi wamemkamata mwanamziki huyo mweye umri wa miaka 62 baada ya kutoa wimbo ambao wachambuzi nchini humo wanasema kwamba tafsiri yake inamdalilisha rais wa sasa Felix Tshisekedi, japo wimbo huo hautaji mtu yeyote.

Ujumbe katika wimbo huo kwa jina 'Ingratitude' unamlenga mtu ambaye amepewa kila analotaka maishani, lakini amekosa kufanya mema wakati yupo madarakani.

Produza wake Claude Mashala amesema kuwa, mwanamuziki huyo alichukuliwa na makachero wa Idara ya Usalama wa Taifa baada ya wimbo huo wenye utata kuchapishwa mtandaoni mwishoni mwa wiki.

Naye mwanamuziki mwenzake, Lofombo Gode amesema, Muana amekamatwa akiwa mjini Kinshasa kwa madai kuwa anapaswa kwenda kutoa tafsri juu ya wimbo huo ambao unaonekana kumvunjia mkuu wa nchi heshima.

Muana ambaye ana uhusiano wa karibu na familia ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Joseph Kabila anadaiwa kutoa wimbo huo wakati ambapo kuna hali ya sintofahamu baina ya viongozi wanaomuunga mkono Rais wa sasa na aliyeondoka.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news