Zuchu atwaa tuzo ya mwanamuziki bora Afrika

Msanii chipukizi na Mtanzania, Zuchu Otuman ametwaa tuzo ya msanii bora chipukizi Afrika kutoka African Music Magazine Awards (AFRIMMA), anaripoti Mwandishi Diramakini.

Zuchu ambaye ni mtoto wa malkia wa nyimbo za taarabu nchini, Hadija Kopa hii ni tuzo yake ya kwanza ya Kimataifa tangu ajiunge na lebo ya WCB Aprili 8, 2020 na tayari kazi zake zimeendelea kufanya vizuri ndani na nje ya Tanzania.

Miongoni mwa nyimbo za Chuchu zinazobamba zaidi kwa sasa ni pamoja na Wana, Raha, Nisamehe, Kwaru, Mauzauza, Shindua, Hakuna Kulala na Asua ambayo amemshirikisha Mbosso pia kutoka WCB
.

Post a Comment

0 Comments