Diamond Platinum atwaa tuzo nyingine Kimataifa

Nyota wa Kimataifa katika Bongo Fleva na Mtanzania, Nasibu Abdul Juma Issack (Diamond Platinum) ambaye anatajwa kuwa ana mafanikio makubwa zaidi katika tasnia ya muziki na mfanyabiashara aliyewekeza katika miradi mbalimbali nchini ikiwemo vyombo vya habari ameendelea kujizotea tuzo mbalimbali, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Diamond Platinunm aliyezaliwa Oktoba 20, 1989 ametajwa tena kuwa Mwanamuziki Bora wa kiume Afrika Mashariki ambapo amepatiwa tuzo ya @afrimawards@afrimma.

Hiyo ni kati ya tuzo nyingi za Kitaifa na Kimataifa ambazo ametunukiwa ikiwemo Channel O, MTV Awards, Soundcity, Kilimnjaro Music Awards, Headies, Afrima, Afrimma, Kora, AEA, the HiPipo Music Awards.

Post a Comment

0 Comments