Mwanamke ajifungua kuku Kituo cha Afya Uvinza

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, mwanamke mmoja wilayani Uvinza Mkoa wa Kigoma uliopo Magharibi mwa Tanzania, amejifungua kuku katika Kituo cha Afya Uvinza baada ya kufika kituoni hapo akidai anapata maumivu ya tumbo, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Dkt. Simon Chacha ambaye ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Dkt.Chacha amesema tukio hilo limetokea asubuhi ya Desemba 6, 2020 baada ya mama huyo kufika katika kituo cha afya akiwa na mume wake huku akiwa na maumivu ya tumbo.

"Baada ya muda wauguzi walitoa kuku katika sehemu ya uzazi ya Mama huyo ambapo hakuna damu zilizoendelea kutoka zaidi ya uchafu tu unaotoa harufu mbaya." amesema Dkt. Chacha.

Pia amedai, tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina kwa kuwa vipimo vinaonyesha mama huyo hakuwa na dalili yoyote ya ujauzito na haoneshi kama alikuwa na ujauzito.

Dkt.Chacha amesema, baada ya kutolewa kuku huyo mama huyo ameendelea kutoa harufu mbaya katika sehemu hiyo ya uzazi na alikuwa na homa kali.

Hata hivyo amemuagiza mganga mfawidhi ampeleke hospitali ya Rufaa Maweni kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi.

Wachambuzi wa masuala ya imani wameidokeza Diramakini kuwa, hizi ni nyakati zenye mfanano na zile za mwisho, hivyo binadamu wasishangae kuyashuhudia mambo ya namna hiyo, badala yake waendelee kusugua magoti kumlilia Mungu na kuishi katika misingi ya neno na maombi.

Ndugu Mwandishi Diramakini rejea maandiko Matakatifu katika Biblia kitabu cha 2 Timotheo 3-9 na hizi ndizo hatari za siku za mwisho;

3 Lakini fahamu jambo hili: kwamba siku za mwisho kutakuwa na nyakati za taabu. 

2 Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, watukanaji, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio na utakatifu; 

3 wasio na ubinadamu, wasiopenda kusuluhishwa, wachonganishi, walafi, wakatili, wasiopenda mema; 

4 wasaliti, wasiojali kitu, waliojaa majivuno, wapendao anasa badala ya kumpenda Mungu. 

5 Hao ni watu ambao kwa nje wataonekana kuwa wana dini, huku wakikana nguvu ya imani yao. Jiepushe na watu wa jinsi hiyo.

6 Maana miongoni mwao wamo wale waendao katika nyumba za watu na kuwateka wanawake dhaifu waliolemewa na dhambi na kuyumbishwa na tamaa za kila namna. 

7 Wao humsikiliza kila mtu lakini hawawezi kutambua kweli. 8 Kama vile Yane na Yambre walivyopin gana na Musa, kadhalika watu hawa nao wanapingana na ile kweli. Ni watu wenye akili potofu, wenye imani ya bandia. 

9 Lakini hawatafika mbali, kwa sababu ujinga wao utakuwa dhahiri kwa watu wote, kama ulivyokuwa dhahiri ujinga wa hao watu wawili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news