Magazeti leo Januari 12,2026

Makumbusho ya Taifa ya Tanzania (NMT) imepokea zaidi ya watalii 100 walioingia nchini kupitia meli ya kifahari ya utalii (Cruise Ship), ziara hiyo ni uthibitisho wa kuimarika kwa sekta ya utalii wa kitamaduni na juhudi za Serikali katika kufungua na kukuza masoko mapya ya utalii.
Watalii walitembelea vituo mbalimbali vya Makumbusho ya Taifa kwa lengo la kujifunza historia, utamaduni na urithi wa Taifa la Tanzania.

Makumbusho ya Taifa la Tanzania inaendelea kujipanga kutoa huduma bora na zenye viwango vya kimataifa ili kukidhi ongezeko la watalii wanaotarajiwa kuendelea kuingia nchini katika msimu huu wa utalii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here